.

Humanitarian Network Wahimiza Serikali Kutatua Hali ya Ukame Nchin

User Rating: 5 / 5

Star ActiveStar ActiveStar ActiveStar ActiveStar Active
 

Serikali imetakiwa kuangazia Kwa undani swala la ukame katika kaunti 23 zilizoathrika na hali ya ukame nchini watu milioni 2.5 wakiathrika. Kulingana na Jane Wariwe kutoka Samburu Women Trust chini ya mwavuli wa ASAL Humanitarian Network (AHN)

ametaka serikali kushirikisha jamii zilizoathrika katika programu kama vile ununuzi wa mifugo Yao ama nyama na tume Kenya meet Commission ,msaada wa vyakula na hata usambazaji wa raslimali muhimu zinazofanya jamii kuzozana maeneo hayo.
‘‘Kwa sasa wengi wameathirika na itakuwa vigumu hali ikiendelea kuwa hivi.Kina mama wetu na watoto wameathirika zaidi kwani ukosefu wa chakula,vituo vya afya hatuwezi fika na hata lishe kwa mifugo ni shida.’’ Jane alisema. Jane anasema kuwa wengi wa kina mama na watoto wameathirika na wameshindwa kabisa kupata huduma za Afya,na hata vyakula haswa wale wajawazito.
Wametaka serikali Za kaunti pia kushirikisha wenyeji katika kaunti hizo katika mazungumzo Ili waweze kuimarisha usalama Kwani wengi wanapigania raslimali kama vile maji na mahali pa kulisha mifugo.
‘‘Serikali za kaunti ziwe mstari wa mbele kuhakikisha kuwa wanashirikisha jamii katika mpango mzima wa kuhakikisha kuwa ukame na baa la njaa hauleti vurugu baina yao.’’ Aliongeza.